Taarifa zinasema kuwa aliyekuwa Sheikh
mkuu wa mkoa wa Mara Othman Magee,amefariki dunia usiku huu akiwa katika
matibabu hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam ambako alikuwa
amelazwa akisumbuliwa na saratani ya kibofu.
Awali marehemu Sheikh Othman Magee alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Bugando na ugonjwa ulipomzidia alihamishiwa Muhimbili.
Shughuli mbalimbali na taratibu za mazishi zimeanza kufanyika nyumbani kwake mtaa wa Kennedy kata ya Mviringo, Musoma mjini ambapo mazishi yanategemewa kufanyika kesho kutwa mjini humo.

INNALILLAHIWAINNAILAIHIROJIUN.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment