MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday, 27 January 2014

Syria: Wajumbe waafikiana kuhusu Homs


Mazungumzo ya amani kuihusu Syria yanayoendelea mjini Geneva yanatarajiwa kuingia siku ya nne hivi leo Jumatatu, ili kujaribu kuyajibu maswali makubwa ya kisiasa kama vile sala linalozua utata la kukabidhi madaraka.

Lakini mazungumzo ya leo yataangazia pia maswala ambayo hayajapata suluhu kama vile kuruhusu misafara ya magari yanayobeba misaada ya chakula kuingia maeneo yaliyozingirwa na majeshi ya serikali katika mji wa kale wa Homs. Hapo jana Jumapili ujumbe wa serikali ya Syria katika mazungumzo hayo ulikubali kuwaruhusu watoto pamoja na wanawake kuondoka katika mji huo.

Akitoa hakikisho hilo Naibu waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Syria Faisal Mikdad alisema kuwa serikali ya Syria iko tayari kuwaruhusu watoto pamoja na wanawake kuondoka akisema kuwa Serikali iko tayari kuwapokea na kuwapa misaada ya madawa, makao na mahitaji mengine ya kimsingi ikiwa makundi ya wapiganaji ambayo aliyataja kuwa 'magaidi' yatawaruhusu kuondoka.

Na katika hatua muhimu ya kuleta afueni katika mji huo wajumbe wa upinzani wamesema kuwa wapiganaji waliopo eneo hilo wataweka silaha chini kuruhusu misaada ya kibinadamu iwafikie maelfu ya raia. Lakini baadhi ya viongozi wa upinzani wameelezea tashwishi kuhusiana na pendekezo hilo la serikali na kutaka hakikisho kwamba hakuna mtu atakayekamatwa na kuzuiliwa. Mjumbe kutoka baraza la kitaifa la upinzani nchini Syria Obeida Nahas amesema hatua hiyo ni muhimu.

MWANA HARAKATI

No comments: