Ni chama cha mapinduzi CCM pamoja na chama demokrasia na maendeleo CHADEMA.
Picha juu katikati ni mwenyekiti wa UVCCM mkoani Kagera, YAHYA KATEME, ambaye amesema kuwa wamepitita ripoti ya CAG, na kujiridhisha katika taarifa hiyo, hivyo wameungana na wananchi pamoja na viongozi ndani ya chama hicho, walioshiriki kufanikisha upatikanaji wa ubadhilifu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo anaotuhumiwa nao aliyekuwa Meya wa manispaa ya Bukoba.
Picha juu aliyebana mikono katikati, ni Katibu wa CHADEMA manispaa yA bUKOBA, bWANA RENATUS KILONGOZI (IKENGYA) ambaye amesema kuwa kwa pamoja wanaunga mkono jitihada zilizofanyika kubaini ubadhilifu na kuwezesha kumshinikiza ajiuzulu aliyekuwa Meya wa manispaa ya Bukoba.
Taarifa ya CAG iliyosomwa na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali LUDOVICK UTOH wiki iliyopita, ilibaini utekelezaji wa miradi ya manispaa usiozingatia misingi ya kisheraia na taratibu zisizofuata kanuni, hivyo zaidi ya sh bilion 2 zilibainika kupotea.
Kutokana na taarifa ya CAG, waziri mkuu kupitia naibu waziri wa TAMISEMI, AGREY MWANRY alimtaka meya kujipima na kujiuzulu maramoja, huku akiamuru aliyekuwa mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba Bwana HAMIS KAPUTA afukuzwe kazi na watumishi wengine watatu washushwe ngazi.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment