MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday, 24 January 2014

KAGASHEKI AHUTUBIA WANA BUKOBA BAADA KUPOKELEWA KWA KIDEDEA

 Juu na chini ni msafara wa pikipiki na watembea kwa miguu, wakiongozana na mbunge Kagasheki kuelekea uwanja wa Mayunga, ambapo amepata fursa ya kuwahutubia wananchi.
 Katika mkutano huo, Balozi Kagasheki amesema kuwa ni wakati wa kushirikiana sasa kuhakikisha maendeleo yanatekelezwa na kuwezesha wananchi kupata haki yao iliyofifia kwasababu za watu wachache, huku akisema kuwa waomber Mungu mpaka kuhakikisha waliofanya ubadhilifu wanachukuliwa hatua za kisheria.
 Amesema kuwa kujiuzulu kwake uwaziri wa maliasili na utalii, kuwa hajutii kwani amewajibika kisiasa na kuwajibika huko siyo lazioma ukahusika moja kwa moja na makosa yaliyotokea, hivyo bado anaomba ushirikiano na wananchi.
 Picha chini ni Diwani wa Kata Bilele, IBRAHIM MABROUK, akimkaribisha mbunge Kagasheki akisema kuwa ni lazima washirikiane ili kuwezesha maendeleo.
 Chini ni meya wa zamani, SAMWEL RUHANGISA aliyesisitiza kuwa kila mmoja na haki yakuleta maendeleo na ni lazima waondoe tofauti zao kwani yote yanayowagombanisha ndiyo ya kuwawezesha wananchi wao kunufaika.

 Picha chini ni meneja wa KIROYERA, WILIAM OSWARD RUTTA, akifatilia kwa karibu katika mkutano huo.
MWANA HARAKATI

No comments: