MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday, 24 January 2014

WANANCHI KATIKA MANISPAA YA BUKOBA WALALAMIKIA ZIMAMOTO

 Hiyo ni kutokana na kuambiwa kujaza fomu ambayo wanalipia elfu 40 bila kuwapa ufafanuzi kuwa fomu hiyo inawasaidia nini ilhali hawapewi mtungi wa kuzimia moto wakati wamelipa fedha hiyo.
Kutokana na malalamiko hayo ambayo wananchi wanasema wakihoji wanaelezwa kuwa kila idara imetakiwa kujitegemea, hivyo wanaamini kuwa zimamoto wanatumia njia hiyo kujipatia fedha za kujitegemea bila kujua kama wanawaumiza wananchi.

Akizungumza na mwanaharakati, mkuu wa kituo cha zimamoto manispaa ya Bukoba Sajenti KISAKA, amesema fomu hiyo inatolewa kwa watu wanaokuwa wamekaguliwa na inabidi wailipie, lakini akaahidi kutoa elimu kuhusu fomu hiyo japo itakuwa ngumu wananchi kuielewa kwa watafundishwa kulipia bila kupata huduma.
MWANA HARAKATI

No comments: