
Pamoja na uznduzi wa Calvat hiyo, Balozi Kagasheki amesema lazima wananchi washirikishwe katika uletaji wa maendeleo ambapo bila kuibua hoja zao hakuna kitakachotengenezwa kikaleta tija katika jamii.
Amesisitiza kuwa yaliyojitokeza katika manispaa yanatakiwa kubaki kama historia, kikubwa wananchi na viongozi wao wanatakiwa kufuata utekelezaji wenye tija, huku akiwataka watendaji wa kata na manispaa kutumia vizuri michango ya wananchi wanayojinyima kuchangia maendeleo.
Balozi Kagasheki yupo jimboni Manispaa ya Bukoba, akikusanya maoni ya wananchi kuhusu kero zinazowakabili, ili azifikishe panapohusika, huku akidai kuwa uwaziri ulimtenga na wananchi kutokana na kazi ngumu aliyokuwanayo.
MWANA HARAKATI




No comments:
Post a Comment