Mbunge mmoja wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati, ambaye
alikuwa katika mstari wa mbele kupinga mauaji ya Waislamu nchini humo,
ameuawa kwa kupigwa risasi katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui.
Msemaji wa shirika la kutetea haki za kibinadam la Human Rights Watch, Peter Bouckaert ameonya kuwa hali nchini humo inaendelea kuwa mbaya kila uchao na raia wote wa nchi hiyo ambao ni Waislamu huenda wakalazimika kutoroka katika kipindi cha wiki chache zijazo.
Maafisa wa kutoa misaada ya kibinadam wamesema kuwa watu tisa wamefariki dunia kufuatia mapigano makali na uporaji uliotokea katika mji mkuu jamuhuri ya afrika ya kati wikendi iliyopita.
Ripoti zinasema kuwa watu wawili wanaoaminika kuwa waislamu waliuawa kinyama wakati wa machafuko hayo.
Vita vikali vilitokea siku ya Jumamosi kati ya wanamgambo wa Kikristo na Waislamu Magharibi mwa mji mkuu wa Bangui ambapo majengo kadhaa yaliharibiwa kwa kuteketezwa.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment