Jeshi la polisi mkoani
Simiyu linawashikilia watu tisa wakiwemo wanawake wawili wa kijiji cha
Mwabulimbu wilayani Maswa kwa tuhuma za mauaji ya kikatili ya kina mama wawili
kuuawa na kuchomwa moto kwa kudaiwa kuzuia mvua kunyesha.
Mbali na wanawake hao polisi pia inawashikilia viongozi wakuu wa jeshi la ulinzi wa jadi “Sungusungu” akiwemo Mtemi na Kamanda wake mkuu kwa tuhuma za mauji hayo ya kikatili kwa akina mama hao ambao baada ya kushambuliwa sehemu mbalimbali za miili yao walichomwa moto kwa madai ya kuzuia mvua kunyesha katika kijiji cha Mwabulimbu wilayani hapa.
Kamanda wa polisi wa
mkoa wa Simiyu Charles Mkumbo akiongea na waandishi wa habari jana ofisini
kwake alisema kuwa viongozi waliokamatwa ni Mtemi mkuu wa sungusungu
Ntalage Mabula (50) na Kamanda wake mkuu Sosoma Mamuda (50) wote wakazi wa
kijiji cha Mwabulimbu,kata ya Mwang’honoli tarafa ya Sengerema wilayani
Maswa mkoani hapa.
Wanawake waliokamatwa
kuhusiana na mauaji hayo ni Tabu Mongo (31) na Joyce Kija (30) watuhumiwa wote
ni wakazi wa kijiji cha Mwabulimbu kata ya Mwang’honoli tarafa ya
Sengerema wilayani Maswa.
Akielelezea tukio hilo
kamanda wa polisi alisema watuhumiwa wote walikamatwa februari 4 kufuatia
viongozi hao wakuu wa sungusungu mnamo februari pili mwaka huu,kutoa amri na agizo
la kupiga yowe na filimbi za hatari na kukusanya wananchi waliowapiga na kuwaua
na kuwachoma moto wanawake hao wawili pia wakazi wa kijiji hicho.
Alisema wananchi hao
wakiwa na silaha zao za jadi,marungu,fimbo mawe waliwauwa wanawake
hao na kisha kuwachoma moto, waliofahamika kwa jina la Gilya Chile (70)
na Nyang’au Nyambalya (30) wote wakazi wa kijiji hicho.
Kamanda Mkumbo
alisema kuwa kabla ya mauaji hayo, kijiji hicho na maeneo mengine wilayani
Maswa na hata mkoa wa Simiyu yalikuwa yakikabiliwa na ukame wa mvua kutonyesha,
na inadaiwa kuwa akina mama hao waliomba kuchangiwa gunia moja kila mmoja kwa
vile wanatoka katika ukoo wa kichifu ili mvua iweze kunyesha.
Kutokana na kuwepo kwa hali hiyo Mtemi wa sungusungu kwa kushirikiana na Kamanda wake mkuu wa Sunsungu Sosoma Mamuda (50) pia mkazi wa Mwabulimbu walipiga yowe na filimbi za hatari kuhoji kulikoni akina mama hao kuzuia mvua isinyesha kijijini hapo na ndipo walipoanza kuwaadhibu kwa kuwashambulia kwa silaha za jadi.
Kamanda Mkumbo alieleza kuwa watuhumiwa wote hao watafikishwa mahakani mara baada ya upelelezi kumalizika.
Kutokana na kuwepo kwa hali hiyo Mtemi wa sungusungu kwa kushirikiana na Kamanda wake mkuu wa Sunsungu Sosoma Mamuda (50) pia mkazi wa Mwabulimbu walipiga yowe na filimbi za hatari kuhoji kulikoni akina mama hao kuzuia mvua isinyesha kijijini hapo na ndipo walipoanza kuwaadhibu kwa kuwashambulia kwa silaha za jadi.
Kamanda Mkumbo alieleza kuwa watuhumiwa wote hao watafikishwa mahakani mara baada ya upelelezi kumalizika.
MWANA HARAKATI

No comments:
Post a Comment