Katibu mkuu wa jumuiya ya kujihami NATO Anders Fogh Rasmussen
amemuonya rais wa Afhaganistan Hamid Karzai kuwa 'anacheza' na moto baada ya
kiongozi huyo kukataa katakata kutia sahihi mkataba utakaowaruhusu wanajeshi wa
NATO kuendelea kuhudumu hata baada ya kukamilika kwa muhula waliokubaliana
awali wa mwisho wa mwaka huu.
''mimi na rais Karzai ni marafiki mno lakini sikubaliani naye kwani hatua yake itarudisha nyuma juhudi za jamii ya kimataifa ya kuleta amani Afghanistan.
Unajua kuwa Nato imewekeza kwa hali mali na damu ya majeshi kuilinda Afghanistan nafikiri jamii ya kimataifa inahitaji shukrani sio habari kama hizo.
'' Iwapo Rais Karzai anamipango ya kukataa kutia sahihi makubaliano hayo basi ni sharti ajiandae kugharamia mishahara ya wanajeshi wa Afghanitsn pamoja na polisi kwani NATO imeitengeza jeshi la Afghanistan hadi kufikia idadi ya majeshi laki tatu u nusu .
Serikali ya Afghanistan haina uwezo huo .
Rusmussen aliambia BBC kuwa Majeshi ya Mungano yamewekeza kwa kiwango kikubwa kwa amani ya taifa hilo na hata iwapo Karzai atakataa kuidhinisha mkataba huo anaimani kuwa Rais atakayechaguliwa Mwezi Marchi hatakuwa na budi ilikuweka sahihi.
Gazeti moja lilimnukuu rais Karzai akisema kuwa jimbo la Helmand lilikuwa na amani Hadi majeshi ya Uingereza chini ya NATO yakaingia huko .
MWANA HARAKATI


No comments:
Post a Comment