Wakizungumza kandayaziwa wakazi wa kijiji hicho wamesema hali ya usari ni mbaya kutokana na kutegemea gari moja kwa muda mrefu na kupelekea msongamano mkubwa wa watu .
Aidha Bw Marino layachi ameongezea kuwa pamoja na vyombo hivyo vya usafiri kuwepo bado havikidhi mahitaji kutokukana na kuharibika mara kwa mara.
Nae afisa mtendaji wa kijiji hicho Bw Yohana Mesai amesema wame fikisha swala hilo sehemu husika lakini hakuna utekelezaji wowote ulifanyika na hivyo ameitaka mamlaka ya usafirishaji majini na Nchi kavu (SUMATRA) kuwajali wakazi wa vijijini .
Kwa upande wake Afisa
mfawidhi wa mamlaka ya usafirishaji majini na Nchi
kavu kanda ya kati Dodoma Bw Bahati Musiba
amesema wao wanatambua safari zinazofanywa kutoka Dodoma
mjini kuelekea Izava hivyo amewataka
wamiliki wa vyombo vya usafiri kujitokeza
ili wapewe leseni bure za usafirishaji vijijini.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment