
Ametoa kauli hiyo baada ya kupewa taarifa ya mwanafunzi aliyekosa karo na mahitaji mengine vinavyofikia elfu themanini, ambapo wakati huo mwanafunzi amekosa masomo kwa miezi minne lakini hakuna aliyesaidia kumpatia kiasi hicho ambapo ameamua kumlipia lakini akawasihi wanajamii kusaidia kuchangia elimu kuliko mambo mengine.
Balozi Kagasheki aliyeshika shavu katikati hapa juu, amesema atakaa na walimu na viongozi pamoja na wazazi ili wapange mikakati ya kuwawezesha wanafunzi ambao hawajajiunga na kidato cha kwanza au darasa la kwanza, ili wajue jinsi ya kupambana na suala hilo, ambapo amesema agenda za kuzungumza na wananchi ni masuala hayo wala siyo mambo ya ushabiki kisiasa.
Chini ni moja ya shule ya sekondari katika kata Rwamishenye, ambapo alikaa katika viwanja hivyo na kujadili mikakati mbalimbali lakini kubwa ni kuwasihi wananchi kucha kujadili mambo yaliyo nje na uwezo wao.
MWANA HARAKATI



No comments:
Post a Comment