Katikati Charlie Adam akishangilia na Mark Hughes
baada ya kufunga mabao mawili yaliyoifanya Stoke imalize ukame wa ushindi ndani
ya mechi sita.
MABAO mawili ya Charlie Adam yameipa Stoke City
ushindi wa kwanza kabisa kihistoria dhidi ya Manchester
United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Britannia.
Adam alifunga mabao hayo dakika ya 38 na 52, wakati
bao pekee la United lililofungwa dakika ya 47 na Robin van Persie.
Kiungo mpya wa United, Juan Mata alicheza kwa dakika
zote 90 na hakuweza kuwaepusha Mashetani hao Wekundu na kipigo. United sasa
inabaki na pointi 40 baada ya kucheza mechi 24 na inaporomoka hadi nafasi ya
saba kutoka ya sita.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment