
Mgombea wa Chama cha Mapinduzi
katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo
ameibuka Kidedea kwa ushindi alioupata katika uchaguzi huo mdogo wa Jimbo hilo
baada ya kukaa wazi kwa muda mrefu kutokana na kutenguliwa kwa aliyekuwa Mwakilishi
wa jimbo hilo Mhe. Mansoor Yussuf Himid.
Masimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la
Kiembesamaki Ndg. Suluhu Rashid , akitangaza matokeo hayo baada ya kumalizika
kwa kazi ya uhesabuji wa Kura na kuzijumlisha kura zote zilizopingwa na
Wananchi wa Jimbo hilo.
Akitangazo matokea hayo ya Uchaguzi
mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki yalioshirikisha Vyama Sita vya Siasa
vilivyosimamisha wagombea wake.
Msimamizi wa Uchaguzi Ndg. Suluhu
akitoa matokeo hayo Mgombea wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Mahmoud Thabit Kombo
ameshinda kwa Kura 1856, sawa na asilimia 75.1 na kutangazwa mshindi wa
Uchanguzi huo Mdogo wa jimbo hilo kuchukuwa nafasi ilioachwa wazi na Mhe.
Mansoor Yussuf Himid, aliyevuliwa Uwanachama na CCM na nafasi hiyo kuwa wazi
kwa muda hadi kufanyika kwa uchaguzi mdogo leo na kumpata mrithi wa kiti hicho.
Mgombea wa Chama cha CUF Mhe.
Abdulmalik Juma Jecha, amepata kura 445, sawa na asilimia 18.3, Mgombea wa
Chama cha ADC Mhe. Amani Ismail Rashid amepata kura 84, sawa na asilimia
3.5, Chama hichi ni kipya kimeungwa na Viongozi walioondoka CUF, na hii ni mara
ya pili kushiriki Uchanguza tangu kuazishwa kilishiriki uchaguzi wa kwanza
kisiwani Pemba katika jimbo la Chambani,Pemba.
Nae Mgombea wa Chama cha
CHADEMA Mhe. Hashim Juma Issa,amepata kura 34 sawa na asilimia 1.5,
katika uchaguzi huo mdogo wa jimbo la kiembesamaki.Mgombea wa TADEA Ali
Mohammed Ali (Mbongo) amepata kura 6 sawa na asilimia 0.3. Nae Mgombea wa Chama
cha SAU Mhe. Ramadhani Simai Mwita amepata kura 1 sawa na asilimia 0.1
Kwa matokeo hayo Tume ya Uchaguzi
Zanzibar imemtangaza Mgombea wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Mahmoud Thabit Kombo
kuwa ni Mshindi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki na anakuwa
Mwakilishi halali baada ya ushindi huo.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment