MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 2 February 2014

MJI WA SIBUT WAKOMBOLEWA, RAIA WAFA NJAA S KUSINI HUKU UCHAGUZI WAGHUBIGWA NA VURUGU THAILAND

Kamanda wa kikosi cha amani cha Umoja wa Afrika katika Jamhuri ya Afrika ya Kati anasema askari wake wameukomboa mji wa Sibut, kutoka kwa wapiganaji wa zamani wa Seleka.

Kamanda huyo, Jenerali Tumenta Chomud, alisema askari kutoka Gabon sasa wako mjini Sibut, na watawanyang'anya silaha wapiganaji waliouteka mji huo Alkhamisi.

Wapiganaji wa zamani wa Seleka - wengi wao Waislamu - wamekuwa wakiondoka mji mkuu, Bangui, ambao uko kama kilomita 200 kusini ya Sibut.
Kuondoka kwa Seleka kumezusha mauaji ya kulipiza kisasi, na watu zaidi ya 40 wameuwawa mjini Bangui katika siku chache zilizopita.
Uchaguzi mkuu ncini Thailand umeanza leo huku ilinzi ukiwa umedhibitiwa, na kukiwa na taarifa za vurugu katika baadhi ya maeneo.
Umoja wa mataifa unakadiria kwamba takriban watu millioni 3.7 nchini Sudan kusini wanakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi walio watiifu kwa aliyekuwa makamu wa Rais Riek Machar.

Mratibu wa maswala ya kibinaadamu katika umoja huo Toby Lanzer amewaambia waandishi habari kuwa mzozo huo ulioanza mwezi Disemba mwaka jana umeharibu masoko pamoja na maisha ya kawaida ya watu, mbali na kusababisha hali mbaya ya kibinaadamu kwa thuluthi moja ya idadi ya raia.
MWANA HARAKATI

No comments: