MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday, 22 February 2014

MWANAFUNZI ALIYESHIKA NAFASI YA TATU KITAIFA AZIMIA BAADA YA MATOKEO


Ni Joyceline Marealle wa Shule ya Sekondari Canossa ya Dar es Salaam. 

Dar es Salaam. Mwanafunzi aliyeshika nafasi ya tatu kwa ufaulu kitaifa katika Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne wa 2013, jana alipoteza fahamu kwa muda baada ya kupata matokeo hayo.

Mwanafunzi huyo, Joyceline Marealle wa Shule ya Sekondari Canossa ya Dar es Salaam, alipatwa na mkasa huo muda mfupi baada ya mwandishi wa gazeti hili kumpigia simu na kumweleza matokeo hayo.

Baada ya kupigiwa simu yake ya mkononi iliyopokelewa na mama yake mzazi (Caroline Munuo), ambaye alisema mtoto wake hajapata taarifa hiyo na kumtaka mwandishi aitoe mwenyewe kwa binti huyo kisha kumpa simu hiyo Joyceline.

Baada ya binti huyo kupewa simu na kuanza mazungumzo na mwandishi alisema: “Naomba usiniambie! Ni kitu kikubwa Mungu amenifanyia.”

Joyceline aliyesikika akitamka maneno hayo huku akilia ghafla sauti yake ilikatika na kukaa kimya kwa sekunde kadhaa, kabla ya mama yake kuchukua simu hiyo, ambapo alieleza kuwa binti yake anaishiwa nguvu.

“Naomba umpigie simu baadaye ameishiwa nguvu anataka kuanguka,” alisema mama huyo wa Joyceline.

Mama yake alisema alitegemea matokeo hayo kwa sababu binti yake na mwenzake ambao ni pacha wamekuwa wakifanya vyema kwa kushika nafasi mbili za kwanza darasani.


(Chanzo ni Gazeti Mwananchi)

MWANA HARAKATI

No comments: