Nicolaus Mac (None Association Movement) KWA MATANGAZO YA REDIO NA TV WASILIANA NASI KWA +255767814844- nicolausngaiza@gmail.com.
Saturday, 22 February 2014
WAUGUZI WAFUKUZWA KAZI KWA KUNYANYASA WAGONJWA
Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, imemtimua kazi muuguzi mmoja na mwingine kumshusha madaraja baada ya kugundulika kushiriki vitendo vya rushwa na kunyanyasa wagonjwa.
Wauguzi hao ambao majina yao yanahifadhiwa wanadaiwa kwa kipindi kirefu walikuwa wakituhumiwa kupenda kuomba rushwa kutoka kwa wagonjwa na kwamba pia walionyesha dhahiri kuwanyanyasa walioshindwa kutoa rushwa.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, alisema kwamba, muuguzi aliyetimuliwa kazi alikuwa chini ya mamlaka ya hospitali yake.
Alisema muuguzi mwingine ni mfanyakazi wa siku nyingi ambaye ameshushwa vyeo na sasa atakuwa anafyeka majani na kupalilia maua. Awali ilisemekana, wauguzi hao walilalamikiwa na wagonjwa na kubainika ni kweli baada ya kuundiwa kamati ambayo ilitimiza wajibu wake.
Uchunguzi wa kamati ulibaini kuwapo kwa matukio mengi yaliyowahusisha wauguzi hao na kwamba ndipo hatua za kinidhamu zilipochukuliwa dhidi yao baada ya kuhojiwa.
Naye Katibu wa Hospitali hiyo, alisema uongozi hautakubali hospitali hiyo ichafuliwe na wafanyakazi wachache.
MWANA HARAKATI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment