Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania,
mheshimiwa JAKAYA MRISHO KIKWETE, amemteua bwana TOGOLAN I. MAVURA kuwa
msaidizi wa rais (hotuba) kuanzia februari 8 mwaka huu 2014.
Taarifa iliyotolewa jana jumanne
jijini da es salaam, na katibu kiongozi Balozi Omben Sefue,inasema kuwa bwana
Mavura anachukua nafasi ya bwana Msafiri Marwa amabaye amehamishiwa wizara ya
mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa na kupangiwa kazi nyingine.
Kabla ya uteuzi huo, bwana Mavura ambaye
ni ofisa wa mambo ya nje alikuwa katibu wa waziri wa mambo ya nje na
ushirikiano wa kimataifa.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment