
Mkurugenzi Mtendaji wa
BUWASA, mhandisi Chaggaka Kalimbia
amesema wateja elfu 87 katika manispaa ya Bukoba wanatarajiwa kuunganishiwa huduma ya maji safi
na Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira -BUWASA- ifikapo Juni mwaka
huu, baada ya kukamilika kwa mradi
mkubwa wa maji.
Amesema kuwa baada ya
wateja hao kuunganishiwa, watakuwa
wanapokea maji kutoka kwenye tanki zilizojengwa eneo la Kashura na Magoti, na
kuwa tanki hizo zitakuwa na uwezo wa kubeba lita milioni tatu na laki saba.
Mhandisi Kalimbia
amefafanua kuwa kufikiwa kwa wateja hao,
matumizi ya maji katika manispaa ya Bukoba yataongezeka hadi kufikia lita
milioni 11 laki mbili na elfu 37 kwa siku tofauti na lita milioni nane na laki
mbili kwa sasa.
Amesema kukamilika kwa mradi huo, kutawezesha kuzifikia kata nne ambazo zilikuwa
hazijafikiwa huduma ya maji safi na salama, ambazo ni Kagondo, Kahororo, Nyanga
na Buhembe.
Mkurugenzi huyo amesema
kuwa hadi kukamilika kwa mradi huo zaidi ya shilingi Bilioni 27 milioni 528 na laki tatu
zinatarajiwa kutumika.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment