Mkuu wa kanda ya Kagera Bi. Pudensiana Rwezaula, (picha chini aliyesimama) amesema kuwa mradi wa jengo hilo umekamilika kwa kiwango kizuri ukiwa na tank la maji, huku akisikitishwa na kuchelewa kukamilika kwa vifaa vya kujengea choo na nyumba za waganga vinavyotakiwa kujengwa na serikali kwa ushirikiano na wananchi kwa mujibu wa makubaliano kuwa wamechelewa kukamilisha vitu hivyo.
Picha chini ni mgeni rasmi wapili kulia, Alhaj Swaibu Mfuruki, akiteta jambo kabla ya kuweka jiwe la msingi la jengo hilo, wa kwanza kulia ni Dokta wa wilaya, wa kwanza kushoto ni mkuu wa vituo vya worldvision (ADP) wilayani Muleba Bw. Prosper Mujungu, na mwenye shati la Pinck ni diwani wa kata Bisheke.
Picha juu ni mtoto akikinga maji kutoka Tnak la maji ya mvua lililopo kwenye jengo hilo la zahanati, na chini kulia ni Prosper Mujungu, akifanya ukalimani katika hotuba fupi ya Mic Nelson mwakili wa Worldvision kutoka Uswis.
Picha juu ni Dokta wa wilaya Muleba Joseph Kisala, akithibitisha kutoa ushirikiano wa kitabibu kwa zahanati hiyo, na chini ni Mac Ngaiza kulia nikifanya mahojiano na mwananchi mmoja, ambaye amesema kuwa hali ya umaskini ni ya kiwango kikubwa kwa wakazi wa maeneo hayo hivyo kushindwa kufika kwenye vituo vya tiba kutokana na umbali, hivyo zahanati hiyo ni msaada mkubwa kwao.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment