MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday 28 February 2014

RUSHWA MANISPAA BUKOBA; TAKUKURU YAKUTANA NA WAZEE

TAKUKURU yaitaka jamii imetakiwa kuelewa kuwa kuporomoka kwa maadili kunasababisha uwepo wa rushwa nchini.
AFISA MKUU TAKUKURU MKOANI KAGERA AKIZUNGUMZA NAMI
 
Mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU, Bwana JOSEPH MWAISWELO, katika semina maalumu ya maadili kwa wazee wa manispaa ya Bukoba, katika mpango wa taasisi hiyo nchi nzima kuhakikisha waelimisha kuhusu maadili ambapo mwaka huu wameanza na wazee.
Amesema kuwa pamoja na maadili, umasikini pia unasababisha kuongezeka kwa rushwa hivyo TAKUKURU imetambua hayo na kuamua kuanza na wazee ambapo pia wanashughulika na wanafunzi wa shule za msingi
Bwana Mwaiswelo amesema kuwa rushwa nchini inaongezeka, hivyo jamii itambue kuwa ni lazima maadili yazingatiwe, huku baadhi ya wazee waliopewa semina hiyo na kutoa michango yao, ni pamoja na shekh wa mkoa ARUN KICHWABUTA,(hayupo pichani) aliyesisitiza kuwa malezi bora ndiyo njia pekee ya kusaidia kizazi cha sasa, ambapo amewata wazazi na walezi, kuwapa ushirikiano wa kutosha walimu kuhusu watoto wao.

Katibu wa CCM manispaa ya Bi JANET KAYANDA,(hayupo pichani) kwa upande wake amesema kuwa jambo la maadili siyo nla sekta Fulani, bali serikali madarakani, wanasiasa na wataalamu pamoja na mwananchi mmoja mmoja wanatakiwa kushirikiana pamoja, kwani akili inaendana na maadili.

 Pichani ni ANNET MWAKATOBE, mkuu wa dawati la elimu TAKUKURU mkoani Kagera.
MWANA HARAKATI

No comments: