Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Bukoba mkoani Kagera GAD MJEMAS amewataka mawakili kutotoa mapingamizi yasiyo ya lazima ili kuhakikisha haki inatendeka kwa wakati.
Hatahivyo viongozi wa magereza wametakiwa kutoa ushirikiano kwa kufikisha faili za kesi za watuhumiwa kwa wakati ili haki itolewe kwa wakati.
Wakati huo huo Jaj MJEMAS amesema kuwa ni muhimu kuajiri mawakili wa kutosha ili kupunguza malimbikizo ya mashauri mahakamani huku akisema kuwa wadau muhimu kwenye sheria ni mashirika binafsi kama MUHOLA na mawakili binafsi pamoja na wananchi wenyewe.
Ni maadhimisho yanayoendelea sasa hivyo tutakuletea habari zaidi.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment