Jaji MJEMMAS amesema kuwa baadhi ya Watu wamekuwa
wakipoteza haki zao kwa kukosa uelewa kuhusu masuala ya sheria, huku baadhi yao wakipoteza muda kwa
kufungua mashauri mahakamani
yasiyostahili.
Akitolea mfano, Jaji MJEMMAS amesema kuwa mwananchi
mmoja, ambaye hakumtaja jina, alifika mahakamani kwa nia ya kumfungulia kesi ya madai baba yake mzazi ambaye bado yuko hai, akimdai Mirathi.
Amesema kuwa Mirathi hutolewa kwa kuzingatia matakwa ya mtoa Wosia, hivyo endapo mwananchi
huyo angekuwa na uelewa wa sheria,
asingepoteza muda wake kufika mahakamani.
Jaji MJEMMAS pia amewataka Wananchi mkoani KAGERA kushirikiana
na Polisi pale unapofanyika upelelezi kwa makosa ya jinai, na pia wajitokeze
kutoa ushahidi mahakamani pale kesi inapoanza kusikilizwa.
Maadhimisho ya Siku ya Sheria Tanzania huashiria kuanza kwa Mwaka
wa shughuli za Mahakama nchini.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment