Anaitwa Rukia
Fungameza umri miaka 20 na mkazi wa mtaa wa Ilembo Kata ya Iwambi Anaetuhumiwa kutupa
mtoto chooni
Picha chini, mwenyekiti wa mtaa
huo Juma Mbuza mwenye Flana ya bluu akiwa na balozi kushoto na mashuhuda
wengine wakimsikiliza mwenyekiti huyo
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina
la Rukia Fungameza[20]mkazi wa mtaa wa Ilembo Kata ya Iwambi anashikiliwa na
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya kwa tuhuma za kutupa chooni kichanga jinsi ya
kiume na kusababisha kifo chake.
Mwenyekiti wa mtaa huo Juma Mbuza
amesema walimtilia shaka mtuhumiwa Februari 18 mwaka huu katika klabu ya pombe
za kienyeji baada ya kutoonekana na ujauzito,ndipo walipomuuliza kulikoni naye
kudai kuwa amejifungua lakini mtoto yupo nyumbani.
Kauli hiyo haikumridhisha Mwenyekiti
huyo ndipo alipoamua kumtafuta balozi wake aitwae Daud Dule na kumuuliza mtoto
yupo wapi ndipo alipoanza kuwa na wasiwasi hali iliyowalazimu kumkamata kutoa
taarifa kituo cha Polisi Iyunga ambapo kabla ya kufika Kituoni majira ya saa
kumi na moja jioni mtuhumiwa alikiri kujifungua na kutupa kichanga chooni
Februari 18 mwaka huu.
Baada ya taarifa hiyo mtuhumiwa
alikamatwa na kupelekwa kituo kikuu cha kati Febuari 19 ambapo Polisi
hawakuweza kufika eneo la tukio licha ya Mwenyekiti wa mtaa kufuatilia mara kwa
mara kwa mkuu wa kituo cha Polisi Iyunga ambapo alijibiwa kuwa watafika.
Hata hivyo baada ya Polisi kutofika
eneo la tukio kwa siku mbili tangu kukamatwa mtuhumiwa Mwenyekiti wa mtaa
alitoa taarifa katika kikao cha kata Februari 21 kufuatia tukio
lililotukia mtaani kwake na Polisi kushindwa kufika kwenye tukio siku tatu
baada ya tukio hali ambayo ilikuwa kero mtaani kwake.
Polisi walifika eneo la tukio Februari
22 majira ya saa tano na nusu asubuhi wakiambatana na Kikosi cha Zimamoto Jiji
la Mbeya ndipo walipoanza anza kuibua mwili wa mtoto ambapo ulikutwa
umeharibika vibaya kutokana na kukaa kwa muda wa siku nne bila kuibuliwa umbali
wa kilometa saba tu kutoka Jijini.
Baada ya mahojiano mtuhumiwa alidai
sababu za kutupa kichanga hicho cha kiume ni kutokana na kuogopa aibu kwa
mumewe aliyepo Songea mkoani Ruvuma kikazi ambapo mimba hiyo aliipata nje ya
ndoa.
Uchunguzi umebaini kuwa mwanamke huyo
aliagizwa na mumewe kurejea Songea mwishoni mwa mwaka jana lakini alikataa
akidai kuwa angeenda mwaka huu baada ya kumsaidia kaka yake shughuli za palizi.
Kabla ya kichanga kilichotupwa chooni
mtuhumiwa ana mtoto mwingine jinsi ya kike anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka
miwili na nusu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa
amelilalamikia Jeshi la Polisi kwa kutoenda eneo la tukio mapema hali ambayo
inasababisha wananchi kujichukulia sheria mkononi hali ambayo inweza kuepukika.
Baadhi ya mashuhuda akiwemo mama Emilly
Amnoni na Paulo Mbawala wamelaani vikali kitendo kilichofanywa na mwanamke huyo
kwani wamedai ni cha kinyama na ni cha kwanza mtaani kwao hivyo wanaomba sheria
iweze kuchukua mkondo wake ili kukomesha kabisa vitendo vya kikatili Mkoani
Mbeya.
Taarifa kwa hisani ya EDDY
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment