Wameongeza kuwa wamekuwa wakikatwa kiasi cha fedha kwa ajili ya mfuko wa jamii NSSF, ambapo hawajawahi kupewa taarifa kuhusu mfuko huo na baada ya kufuatilia wameambiwa hakuna majinayo kwenye shirika hilo, hivyo kiasi kinachokatwa wanataka kujua kinapelekwa wapi na mwajiri wao.
Kutokana na madai hayo, wamegoma kuingia kazini, hadi mwajiri wao awalipe fedha zao ambazo wanasema pamoja na kuwa azikidhi ugumu wa maisha zingewasaidia kujikimu baadhi ya mahitaji muhimu.
Akizungumza nasi baada ya kufika katika ofisi hiyo, Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya KSSA bwana ALBOGAST LUGAIMUKAMU, amesema kuwa ni kweli wafanyakazi hao(walinzi) wanamdai mishahara ya miezi mitatu, na leo anaanza kuwalipa kidogo kidogo ili amalize deni lao, huku akiwaomba kuingia kazini kwani anatambua deni lao, ambalo hatahivyo hakufafanua ni kwanini amekuwa hawalipi tangu awali.
Kuhusu suala la NSSF hakutoa ufafanuzi wa jambo hilo, japo tumewatafuta maofisa wa NSSF ambao wamekili kuwa hawana mafungu ya wafanyakazi hao, lakini wameshapokea malalamiko yao na wanaendelea kuyafatilia ili watupe undani wa mstakabali wao.
Bwana Albogast Lugaimukamu.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment