Taarifa zinasema kuwa basi la
kampuni ya Japanese Express linalofanya safari zake kati ya Makete - Njombe,
limetumbukia kwenye mto katika eneo la Lwamadovela wilayani Makete.
Basi hilo lilikuwa likitokea Njombe
kuelekea Makete na ajali hiyo imetokea majira ya saa 11 jioni kwa mujibu wa
mashuhuda wa ajali hiyo
Hatujapata taarifa za vifo lakini baadhi
ya abiria waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hospitali ya Ikonda Consolata

No comments:
Post a Comment