Jamaa za abiria wa ndege hiyo wamekumbwa na majonzi makubwa.
|
Mamlaka ya usalama wa safari za baharini nchini Australia
imesema kuwa operesheni ya kuitafuta ndege ya shirika la Malaysia iliyotoweka
imesitishwa kutokana na hali mbaya ya hewa na mawimbi makali baharini.
Taarifa zinasema kuwa upepo mkali pamoja na mvua kubwa inayonyesha katika
eneo hilo ina maana kuwa ndege hazitoweza kupaa kwa usalama. Mawimbi makali
yameilazimisha meli ya jeshi la wanamaji wa Australia kuondoka katika eneo
ambalo mabaki yanayodhaniwa kuwa ya ndege hiyo yalionekana hapo jana Jumatatu.Dr Erik van Sebille, ambaye ni mtaalam wa maswala ya Baharini katika chuo kikuu cha New South Wales mjini Sydney, amefanya utafiti katika eneo hilo la kusini mwa Bahari Hindi kutambua ni wapi na vipi vifusi vinasafirishwa na mawimbi ya bahari. Anasema itakuwa vigumu sana kupata mabaki ya ndege hiyo.
" Ni eneo lisiloweza kukalika duniani, acha niseme. Upepo unaovuma ni mkali sana, mawimbi ni makubwa, ni mojawepo wa mawimbi makubwa zaidi baharini. Unapofika katika eneo hili la kusini, unaanza kuhisi athari za eneo la Antactica kwenye bahari. Hapa tunazungumzia dhoruba kali kali sana hususan wakati huu tunapoingia majira ya kupukutika," anasema Dr. Erik van Sebille.
Kadhalika amesema kuwa vifusi vilivyoenekana hapo jana tayari vimekwishaondolewa katika eneo hilo na mawimbi makali.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment