LEO majira ya sita mchana hadi saa
kumi na moja jioni katika barabara iendayo uwanja wa ndege wa kimataifa KIA
Kilimanjaro International Airport kumetokea machafuko pata shika vuta
nikuvute shati kuchanika rubega kufumuka..!
Takribani kama masaa mawili usalama
ulipotea baada ya Wamasai kudai kufukuzwa katika makazi yao wakiambiwa ni eneo
la uwanja wandege.
Wamasai hao waliamua kuzuia magari
yalioelekea Uwanjani hapo huku wakisema kuwa hata wamiliki wa
uwanja huo nao wahame kwani waliwakuta awali wakiishi hapo.
Polisi na magari ya PT
walifika katika tukio hilo na kutaka kumaliza migogoro hiyo kisheria ila
wamasai wamesema endapo muafaka utalenga kuwakandamiza hawako tayari kuhama.
Na Mwanaharakati.

No comments:
Post a Comment