Singapore umetajwa kuwa mji ghali zaidi duniani kuishi kwa
mwaka 2014 na kuipiku miji mingine 131 kwa mujibu wa taarifa ya Economist
Intelligence Unit (EIU).
Nguvu ya sarafu ya mji huo ikiwa ni pamoja na gharama kubwa
ya uendeshaji magari na kuongezeka kwa malipo ya huduma za umma kumechangia
Singapore kuwa juu ya miji yote duniani kwa ughali wa maisha.
Pia ni mahali ambapo nguo zinauzwa kwa bei ya juu kabisa
kuliko miji yote duniani.
Singapore imechukua nafasi ya mji wa Tokyo, amao ulikuwa
unaongoza kwa ughali wa maisha mwaka 2013.
Miji mingine mitano inayoongoza kwa gharama kubwa za maisha
duniani ni pamoja na Paris, Oslo, Zurich na Sydney, huku Tokyo ukiporomoka hadi
nafasi ya sita.
Mji wa New York unatumiwa kama kigezo cha utafiti wa shirika
la EIU kuhusu gharama za maisha katika miji mbalimbali duniani. Wanaangalia
zaidi ya bei binafsi 400.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment