MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday, 21 March 2014

KIGOGO ANAYEJIHUSISHA NA USHOGA NCHINI TANZANIA ABAINIKA

WAKATI masuala ya ushoga yakipingwa kwa nguvu zote hapa nchini, skendo ya aina yake imeikumba serikali baada ya siri kuvuja kuwa mmoja wa viongozi kumi wa juu nchini ni shoga.
Taric Jumbe akitoa ushuhuda jinsi alivyofanya mapenzi na kigogo huyo.

Habari hizo za kushtua na kufedhehesha taifa ambazo zimefanyiwa kazi na dawati la Ijumaa kwa kushirikiana na kitengo cha OFM cha Global, zilitua hivi karibuni chumba cha habari kupitia kwa kijana aliyejitokeza na kueleza alivyofanya mapenzi ya jinsia moja na kigogo huyo ambaye jina lake linahifadhiwa kwa sasa.

“Mimi naitwa Taric Jumbe, nina miaka 21, nimefika hapa kutoa ushuhuda wangu kuwa nilifanya mapenzi na... (anataja jina), tulianza kuchat kwenye Facebook, akaniomba urafiki, nikamkubalia nikijua ni wa kawaida tu.

“Baadaye akaanza kunitongoza na kuniahidi fedha nyingi, nikakubali. Siku ya kwanza tulikutana Dar, Hoteli ya Serena, akanielekeza chumba alichopo (anataja namba ya chumba), nikaenda na kuwakuta walinzi wake, nilipojitambulisha wakaniruhusu kuingia chumbani kwake. Nimeshafanya naye mara tatu,” alisema kijana huyo.

Ameendelea “Mwanzo nilikuwa nawasiliana naye kwa Facebook lakini tulipozoeana alinipatia namba zake za simu.”

Bila chenga ilibainika kuwa namba hiyo ni ya kigogo huyo, lakini ilipopigwa kwa lengo la kuwasiliana naye moja kwa moja, iliita bila kupokelewa na kuwafanya waandishi kuendelea na kazi ya kumhoji kijana huyo kwa kina.

Jumbe aliweka wazi kuwa siku ya kwanza kukutana naye alilipwa shilingi elfu themanini sambamba na ahadi kuwa wakati wowote atakapokuwa na shida awasiliane na kigogo huyo ambaye msafara wake huongozwa na pikipiki yenye king’ora na gari la polisi, kwa lengo la kuwezeshwa kimaisha.

Aliongeza kuwa kiasi kikubwa alichowahi kuhongwa ni shilingi laki tatu (300,000), huku akiainisha kwamba fedha nyingine alikuwa akipewa kidogokidogo kwa ajili ya kujikimu.

Mbali na kijana huyo kukiri kufanya mapenzi mara mbili na kigogo huyo hotelini, mshangao ulikuja pale alipoweka wazi kuwa mara ya tatu alimfuata kiongozi huyo nyumbani kwake ambako alishirikiana naye tendo hilo la aibu.

Waandishi walipotaka kujua waliwezaje kufanya uchafu huo nyumbani kwa kigogo huyo mwenye familia, Jumbe alisema: “Ni kweli anaishi na familia lakini nje ya nyumba yake ana ofisi, huko ndiko alikonikaribisha na kunifanyia mchezo huo.”
TAHADHARI
Tunapenda kuutaarifu umma kuwa tumeamua kulificha kwa makusudi jina la kigogo huyu ili kuilinda heshima yake ambayo ni kubwa katika jamii yetu. Tutaliweka wazi wakati wowote endapo kati ya mambo haya yatajitokeza.

Mosi, kijana huyo (Jumbe) atadhuriwa. Tunajua nguvu alizonazo mheshimiwa huyu ni kubwa, tunaomba kumfahamisha kwamba tutamuanika hadharani endapo Jumbe atafikwa na matatizo yoyote yasiyo ya kawaida.

Pili, endapo tutathibitisha kuwa anaendelea na mchezo wake huu usiokubalika na mwisho, endapo waandishi waliokwenda kufanya naye mahojiano, ambao yeye na wapambe wake wanawafahamu, watapata madhara yoyote
Chanzo:www.globalpublishers.info
 Na Mwanaharakati.

No comments: