|
Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya
Mtakatifu Monica, Kihonda mkoani Morogoro, Octavian Msimbe akionyesha tunguli
zilizozungushiwa sanda zilizokutwa kaburini kwa marehemu Ngwea.
|
Wakati hati ya kifo cha aliyekuwa rapa bora Bongo, marehemu Albert Keneth Mangweha ‘Ngwea’, ikiendelea kushikiliwa nchini Afrika Kusini alikokutwa na umauti mwaka jana, kwenye kaburi lake kumekutwa tunguli zilizozungushiwa sanda.
Tunguli
hizo zilikutwa Ijumaa ya wiki iliyopita na Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya
Mtakatifu Monica, Kihonda mkoani Morogoro, Octavian Msimbe ambapo ziliibua hofu
miongoni mwa waumini wa kanisa hilo lililopo katika eneo hilo la makaburi.
Awali, ilielezwa kuwa siku hiyo padri huyo
alioteshwa ndoto usiku juu ya uwepo wa vitu vya ajabu katika makaburi hayo
ndipo akakemea kabla ya kwenda kuvishuhudia asubuhi yake (Ijumaa iliyopita)
huku paparazi wetu akinyetishiwa na kuwahi eneo la tukio.
Alipoombwa kutaja majina ya waumini hao alisema:
“Sitaweza kutaja majina yao wala ya kigango yaliyoandikwa kwani wanajijua
wenyewe na mbaya zaidi hata waumini wataona katika ibada Jumapili hii (Jumapili
iliyopita), nitaonesha madhabahuni,” alisema padri huyo ambaye tangu alipofika
kwenye kanisani hilo limekuwa na maendeleo makubwa.
Stori: Dustan Shekidele
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment