|
Wachimbaji wakiandamana leo wilayani Nzega mkoani Tabora.
|
Jeshi la polisi wilayani Nzega mkoani Tabora
limetumia nguvu kusambaratisha maandamano ya wachimbaji wadogo wa madini ya
dhahabu yaliyolenga kupinga kufungwa kwa
machimbo yao ya Mwashina yaliyo jirani na mgodi wa Resolute Tanzania Limited
wilayani Nzega.
Mara baada ya kukaribia katika eneo
la machimbo ambako maandamano yalikuwa yanaelekea,kabla hata hawajafika eneo la
machimbo,ghafla polisi waliibuka na kuanza kurusha mabomu hovyo na baadaye
kumkata mbunge wa jimbo la Nzega Dkt Hamis Kigwangalla ambaye kabla ya kuanza kwa
maandamano hayo alifanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nzega ndogo ili
kujua mstakabali wa wachimbaji hao ambao hivi karibuni waliziuiwa kuchumba na
kamishana wa madini nchini Paul Masanja kwa kile kilichotajwa kuwa wamevamia
eneo hilo.
Kufuatia malalamiko ya wachimbaji
hao kuondolewa bila kujali gharama waliozotumia walimwomba mbunge wao aridhie
maandamano hadi katika eneo la machimbo ndipo mkutano ukavunjika na maandamano
yakaanza na matokeo yake mabomu ya machozi pamoja na risasi za moto.
Katika na purukushani hizo polisi walifanikiwa
kumkamata mbunge huyo na kumjeruhi mtu mmoja kwa risasi ya moto kwenye paji la
uso ambapo waliondoka nae kwenye gari pamoja na mbunge huyo.
Katika hatua nyingine hali ilikuwa
tete kwa waandishi wa habari kwani askari wa jeshi hilo waliziba njia na
kuwazuia waandishi wa habari kufanya kazi zao kwa vitisho mbalimbali na
matumisi ingawa hali hiyo ilitulia baada ya maandamano ya wachimbaji
kujitokeza.
Na
Kadama Malunde-Nzega
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment