Bi. Jeanne na Athuman Juma walianza
kupanda mlima kupitia Kampuni ya Nordic Tours tarehe 18.3.2014 kwa kutumia njia
ya Rongai – Kibo –Marangu safari ambayo ingewachukua siku tano.
Hadi sasa taarifa za awali
zinaonyesha kuwa Bi. Jeanne alitakiwa kwenda kileleni Kibo lakini katika
mazingira yasiyofahamika alibadili uamuzi na kuelekea kilele cha Mawenzi
ambacho huwa hakitumiwi na watalii isipokuwa kwa kujaza fomu maalum
inayoonyesha kuwa mgeni amekubali kwa hiyari yake kupanda kilele hicho.
Shirika la Hifadhi za Taifa kwa
kushirikiana na Kampuni ya Nordic Tours wanaendelea na jitihada za uokoaji kwa
kutumia askari ambao wanaelekea eneo la tukio pamoja na helikopta itakayosaidia
zoezi la uokoaji kwa kutegemea na hali ya hewa itakavyotulia ambapo hivi sasa
kuna mawingu mazito katika eneo la mlima.
Umma utaendelea kufahamishwa
maendeleo ya jitihada za uokoaji kadri zitakavyopatikana.
Imetolewa na Idara ya Mawasiliano
Hifadhi za Taifa Tanzania
Na Mwanaharakati.

No comments:
Post a Comment