MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday, 11 March 2014

SERIKALI YATANGAZA HALI YA HATARI KISIWANI MUSIRA

Ni baada ya uvamizi wa ndege ambao hawajafahamika jina kitaalamu, wanaokunya kinyesi chenye sumu.
Huyu ndiye ndege anayeogopwa.

Ni ndege na mazalio yao
Wataalamu na viongozi kutoka manispaa ya Bukoba wakishuka kwenye mitumbwi.
Huu ndiyo msafara wa viongozi na wataalamu waliowasili kisiwani Musira.
 Ndege hao wanaua kuku na mbuzi, pamoja na kutoboa mabati baada ya kula au kugusa kinyesi chake ambapo serikali ya manispaa ya Bukoba imeamua kupeleka wataalamu kutoka wizara ya afya kitengo cha uchunguzi magonjwa ya binadamu na mifugo.
Afisa Tarafa ABDON KHAWA na mtaalamu kutoka wizara ya afya mwenye nguo ya blue Dk MUNDA ELIAS, akiwaeleza wananchi mikakati inayoanza kisiwani humo.
Mwakilishi wa mkurugenzi manispaa DIDAN SOMBE.
Wananchi wakisikiliza kwa makini
Huyui ndiye aliachwa kulenga shabaha ya kufukuza ndege hao.
Mpaka serikali na wataalamu hao wafika kisiwani humo, kuku 516 na mbuzi 12 wameshapoteza maisha baada ya kula kinyesi cha ndege hao. Hivyo wameweka marufuku ya kupeleka na kutoa au kupelka ndege au wanyama wa aina yoyote kisiwani Musira.
Na Mwanaharakati.

No comments: