| Dokta akidumbukiza kidole kwenye jeraha la mwenyekiti alilochomwa kisu kifuani. |
Vijana wasiofahamika wamchoma kisu cha Mbavu Ndugu
Richard ambaye ni M/Kiti wa Tawi la CHADEMA la Kijiji cha Tagamenda siku moja
tu baada ya Mama Mzazi wa Kijana huyo ambaye alikuwa Mjumbe wa Serikali ya
Kijiji hicho kwa tiketi ya CCM kuamua kuhamia CHADEMA kwa madai ya kuchoshwa na
siasa zisizokuwa na mwelekeo za Chama hicho!!!!
Waka huo huo, DEREVA
wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba, Mohamed Kunambi,
ameshambuliwa na kujeruhiwa na watu wasiofahamika.Tukio hilo limetokea usiku wa kumkia leo eneo la Ifunda jimbo la Kalenga wilaya ya Iringa Vijijini mkoa wa Iringa.
Mbali na dereva huyo diwani wa kata ya Ifunda, Eliya Mngwila, naye amejeruhiwa na watu hao waliposhambulia gari alilopanda.
Hayo yalielezwa jana na Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga, wakati alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maendeleo ya mchakato wa kampeni.
Mtenga alisema tukio hilo lilitokea eneo Ifunda ambapo vijana waliokuwa kwenye gari lenye namba za usajili T 156 CDA iliyokuwa na nembo ya M4C inayotumiwa na chama hicho.
Alisema vijana hao wakiwa na silaha mbalimbali yakiwemo mapangawalimkuta dereva huyo pamoja na viongozi wengine wa CCM akiwemo diwani huyo na kuanza kuwashambulia.
Alisema baada ya tukio hilo waliojeruhiwa walipelekwa Makao Makuu ya Polisi mkoa wa Iringa abako waliandika maelezo na kupewa kibali cha kwenda hospitali (PF3).
"Walishambulia magari yetu kwa kuyavunja vioo hivi sasa yako polisi, tunauhakika waliofanya hivi ni wafuasi wa CHADEMA na hayo ni maelekezo kutoka kwa viongozi wa juu wa chama hicho," alisema.
Kwa mujibu wa Mtenga, gari la CCM lililoshambuliwa ni lenye namba za usajili T 139 CKS ambalo pia liko Polisi.
Wakati huo huo, CCM imesema CHADEMA imeingiza mkoani humo vijana 120 kwa ajili ya kufanya vurugu ili kuvuruga mchakato wa uchaguzi huo.
Mtenga, alisema taarifa za uhakika walizonazo, zinasema vijana hao wameingia mkoani humo juzi na watasambazwa kwenye kata mbalimbali za jimbo hilo.
"Hivi sasa vijana hao wako Iringa mjini wakijiandaa kutekeleza malengo yao ambapo miongoni mwake ni haya yanayotokea sasa," alisema.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment