Hatua hiyo imefikiwa baada ya
mkutano wa wanachama uliofanyika jumamosi machi 8, mwaka huu kwa pamoja
kuazimia kuung'oa madarakani uongozi uliokuwepo baada ya kujadiliana kwa kina
katika mkutano huo
Chama cha demokrasia na
maendeleo CHADEMA kimefikia hatua ya kuchukua maamuzi magumu baada ya kuufuta
uongozi wote wa ngazi ya wilaya ya Makete, na kuuingiza uongozi wa muda ili
kukinusuru chama hicho
![]() |
| Aliyekuwa Mwenyekiti wilaya ya Makete Shaaban Mkakanze |
Miongoni mwa viongozi
waliong'olewa ni pamoja na mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Makete Bw.
Sahaaban Mkakanze na katibu wake pamoja na uongozi mzima uliokuwa ukiongoza
chama hicho wilaya
Mkutano huo ambao pia
uliowashirikisha viongozi wa chadema mkoa wa Njombe akiwemo mwenyekiti Bw.
Lulandala, ulibaini kuwa kasi ya kukua kwa chama hicho wilayani Makete ni ndogo
ukilinganisha na maeneo mengine licha ya jitihada zinazofanywa na ndiyo maana
wakaona wabadilishe uongozi
Katika mkutano huo waliazimia
kuchagua uongozi wa muda ambao umepewa miezi miwili ya matazamio kuhakikisha
wanakiimarisha chama katika kata zote za wilaya ya Makete ikiwemo kuunda
uongozi wa kila kata ambao unaweza kufanya kazi kama inavyotakiwa
Viongozi wa wa muda
waliochaguliwa kushikilia chama hicho ngazi ya wilaya kwa muda ni Bw. Ibrahim
Ngogo ambaye ni mwenyekiti, Bw. Ilomo ambaye ni katibu na Bw. Stephano Kasanga
ambaye ni katibu mwenezi
Mkutano huo umewapa miezi
miwili ya kukiimarisha chama kabla ya kuitishwa mkutano mwingine ambao utakuwa
wa uchaguzi wa wanachama kuwachagua viongozi wa wilaya wa kukiongoza chama
hicho.
Na Mwanaharakati.


No comments:
Post a Comment