Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah
Mwambene akizungumza na wabahabari.
SERIKALI imetoa ufafanuzi juu ya vitambulisho
vya waandishi wa habari ( Press card) wakati wa Bunge Maalum la katiba na
kusema kuwa ndicho kigezo pekee kitakachowezesha waandishi wa habari
kutimiza majukumu yao vyema katika kipindi chote cha bunge hilo.Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Assah Mwambene wakati akitoa tamko la Serikali kufuatia taarifa potofu zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini.
Mwambene alibainisha kuwa utaratibu wa kutoa vitambulisho hivyo si mgeni kama ilivyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari na kwamba unaweza kukipata ndani ya saa 24 ikiwa tu mwandishi anakidhi vigezo.
Alisema vitambulisho vinatolewa tu kwa mwandishi mwenye taaluma ya uandishi wa habari kutoka chuo kinachotambulika na Serikali kwa kuzingatia sheria na kanuani zilizowekwa.
Alisisitiza kuwa utaratibu wa kutoa vitambulisho kwa waandishi habari upo na ni wa kisheria hivyo ni lazima ufuatwe.
Na Mwanaharakati.

No comments:
Post a Comment