MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday, 17 March 2014

WAANDISHI JINSI YA KUSHIRIKI BUNGE LA KATIBA

Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo waandishi na wahariri kutoka vyombo mbalimbali nchini.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe Samia Sululu Hassan akifungua warsha ya siku moja kwa wahariri na waandishi wa habari juu ya nafasi ya watetezi wa Haki za Binadamu katika Katiba mpya.
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Ndg. Onesmo Olengurumwa akitoa mada juu ya ya mtazamo na jukumu la wabunge wa katiba na waandishi wa habari za katiba pamoja na watetezi wa haki za binadamu katika mchakato wa kuandika Katiba mpya mkutano wa siku moja uliofanyika mjini Dodoma.

Akifungua warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari kuhusu nafasi ya watetezi wa haki za binadamu na asasi za kirai katika katiba mpya jijini Dodoma, Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe Samia Sululu Hassan amesema waandishi wa habari wana nafasi kubwa ya kuelimisha jamii juu ya haki za binadamu kupitia kalamu zao kwa kuzingatia weledi wa fani yao na maadili ya uandishi.
“waandishi wa habari pamoja na wahariri wao wanaweza kwa kuweka mbele maslahi ya taifa kuripoti na kuandika habari zenye kuleta suluhu, amani, mshikamano na utulivu,” amesema.

Amesema waandishi wa habari kwa kutumia kalamu zao wanaweza kushauri na kushirikiana na serikali na mamlaka zingine kupatikana kwa katiba mpya yenye tunu za taifa,
Sululu aliongeza kwa kuweka hoja zao kwa ari ya utulivu wanaweza kabisa kuleta mshikamano na ushirikiano wa kitaifa katika kudumisha amani na haki za binadamu nchini.
Amesema kwamba kupitia bunge la katiba wanahabari ni kiungo muhimu katika kufikisha ujumbe kwa wananchi na kuelimisha umma jinsi sheria na haki za binadamu zinavyoweza kulinda na katiba ya nchi.

“Rasimu ya katiba haijatambua mahali popote nafasi ya mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotetea haki mbali mbali za raia kama zilivyoanishwa kikatiba,” amesema
Olengurumwa aliongeza kwamba rasimu ya katiba pia haijatambua wasaidizi wa kisheria wakujitolea (Paralegal) ambao wanatoa msaada mkubwa kisheria kwenye ngazi za vijijini.
Amesema ni muhimu kwa watanzania kuendelea kupanua mjadala wa katiba ili misingi ya haki za binadamu iingie kwenye mifumo ya utetezi wa haki za binadamu nchini.

Olengurumwa amesema waandishi wa habari kama vile watetezi wa haki za binadamu maisha yao lazima yalindwe na kutetewa na katiba ya nchi ili kujenga mazingira mazuri ya haki za binadamu nchini.

Hivi karibuni rasimu ya pili ya Katiba ilipendekeza Muungano wa Serikali tatu – Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Tanganyika.
Mjadala wake ulianza, ambapo wasomi walikosoa takwimu za Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu idadi ya waliotoa maoni, kuwa zimetumika kuupotosha umma.

wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sabato Nyamsenda na Bashiru Ally wakati wakizungumza katika kipindi cha Je, Tutafika? kinachorushwa na Channel Ten hivi karibuni.
 Na Mwanaharakati.

No comments: