Kati ya wanafunzi elfu tatu na 353 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu ni wanafunzi elfu moja na 706 ambao mpaka sasa wamejiunga sawa na asilimia 51.

Bi Kajuna amesema wanafunzi elfu moja na 379 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2014 katika Halmashauri ya Karagwe, mpaka sasa bado hawajaripoti kwenye shule walizopangiwa kwa ajili ya kuanza masomo yao.
Aidha amesema kuwa wanafunzi 268 sawa na asilimia nane wamejiunga na shule binafsi .
Bi. Kajuna amesema kuwa kutokana na tatizo hilo, halmashauri ya wilaya hiyo, tayari imeunda kikosi kazi cha kufuatilia watoto hao ili kubaini sababu ambayo imesababisha watoto washindwe kuripoti shuleni na kikosi kazi hicho kitaongozwa na afisa elimu sekondari .
Amefafanua kuwa tayari walimu wakuu wameishaagizwa kutokuwafukuza watoto ambao hawajakamilisha karo na mahitaji mbalimbali ya shule na badala yake wakubaliane na wazazi.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment