Akithibitisha kukamatwa kwa wanawake hao Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma David Misime amesema wanawake hao wanatoka Mikoa mbalimbali nchini na Msako wa kuwakamata umefanyika March 05 mwaka huu majira ya saa tatu usiku katika mitaa ya uhindini na Air Port.
Aidha Kamanda Misime amesema kuwa katika msako huo watu wawili wanaume wamekamatwa wakiwa na mirungi robo kilo katika mtaa wa barabara ya nane Manispaa ya Dodoma ambao ni NASSOR ALLY mwenye miaka 45, Mwarabu mkazi wa barabara ya kumi na AYUBU TEPO mwenye miaka 40, Muarusha, Fundi cherehani mkazi wa Chamwino.
Pia katika Wilaya ya Kongwa kijiji cha
Mlanje kata ya Matongoro amekamatwa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la
SHEDRACK MACHILE mwenye miaka 46, akiwa na Lita 30 za pombe ya moshi akiziuza.
Kamanda Misime amesema msako unaendelea
na amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment