Kamati za ulinzi na usalama katika mikoa ya Kagera na geita,
zimetakiwa kulinda vituo vya dawa na kufuatilia jinsi zinavyopokelewa na
kusambazwa kwa umakini.
 |
Bohari iliyozinduliwa |
Hatahivyo wakuu wa mikoa hiyo wametakiwa kufuatilia kwa
karibu, bila kusubiria ofisini ili wajiridhishe na jinsi utaratibu
unavyofanyika kwani kuna wizi mkubwa wa dawa za serikali katika mikoa hiyo.
Hayo yamesemwa na naibu waziri wa afya Dk KEBWE STEPHEN
KEBWE, katika uzinduzi wa bohari ya huduma ya vifaa ba dawa kwa mikoa ya Kagera
na Geita, iliyozinduliwa katika eneo la MALAHALA wilayani Muleba mkoani Kagera,
itakayohudumia jumla ya vituo 270.
Amesema
kuwa serikali inasikitika kuona dawa za serikali zinapatikana kwenye vituo vya
watu binafsi, huku wananchi wakikosa huduma katika hosptali za serikali, hasa
wilaya ya Ngara ikiongoza kwa upotevu wa dawa.
 |
Naibu waziri STEPHEN KEBWE akikata utepe |
 |
Naibu waziri akipata maelezo ndani ya Bohari hilo |
 |
Kaimu mkurugenzi MSD COSMAS MWAIFYA |
Kwaupande wake mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa
bohari ya dawa nchini, Profesa ALI MTULIA, amesema kituo hiki kitahudumia vituo
vyote vya afya mkoani Kagera, na baadhi ya wilaya za Chato, Bukombe na Mbogwe,
mkoani Geita.
 |
Mwenyekiti wa Bodi ya bohari ya dawa Profesa ALI MTULIA |
Awali, bohari ya mwanza ilikuwa ikihudumia mikoa 6,
halmashauri 37, vituo vya afya na zahanati
elfu moja na 73.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment