![]() |
Kulia ni Mery Msuya katibu TCRA, Frederick Ntobi kaimu TCRA, Lawi Odielo meneja kanda ya ziwa na kushoto ni Jasson Ndanguzi kutoka wizara ya mawasiliano sayansi na teknolojia. |
![]() |
Injinia Lawo Odielo akifafanua jambo kwa wanahabari. |
![]() |
![]() |
Moja ya aina ya King'amuzi ikioneshwa utendaji wake kwa wanahabari |
![]() |
Picha ya pamoja |
Amesema kwa sasa timu nzima ya taifa katika utoaji elimu kwa
UMMA kuhusu mabadiliko ya teknolojia ya mawasiliano nchini, ipo mkoani Kagera
ikitoa elimu jinsi ya wananchi kukabiliana na mabadiliko hayo.
Sambamba na hilo, wameshirikisha wadau wa matangazo zikiwamo
redio zilizoko kwenye eneo husika, na matangazo kwa njia ya gari ambayo
yatakuwa yakipita katika mitaa ya Bukoba kwa ajili ya taarifa hiyo.
Katika mabadiliko hayo, matangazo ya Digitali yatasambaa
kilomita 80 katika eneo husika, ambapo maeneo ya Karagwe yanaweza kupata kwa
kuweka Dish au Antenna nje kulingana na king’amuzi kitakachokuwa kimenunuliwa
na mteja.
Bwana Ntobi, amesisitiza kuwa wanaotumia dishi binafsi na
Cable hawataathirika baada ya mitambo yao kuzimwa, huku akisema kuwa waliokuwa
wakipata TBC kwa njia ya Antenna hao hawataipata kabisa.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment