![]() |
| Baadhi ya waumini wakitoka katika kanisa la MATER MIZEL COMBDIEL mjini Bukoba. |
Hayo yamesemwa na baba askofu msaidizi jimbo
katoliki la Bukoba, muhasham METHODIUS KILAINI, katika ibaada ya ijumaa kuu,
kama kumbukumbu ya mateso ya Yesu Kristo.
Baba askofu Kilaini, amesema kuwa ni siku ya
kumwomba mungu atuhepushe na majanga na uchochezi, huku akisistiza kuwa jamii
ipinge na kukomesha wenye kuwarubuni, kubaka watoto na kuua albino kwa tama ya
fedha.
Katika ibaada hiyo, askofu Kilaini amehimiza
kuwaombea wenye madhambi hayo kutubu, na kama hawatamrudia Mungu wataendelea
kupata matatizo yasiyozuilika, huku akiwataka waumini kuwaombea viongozi wote
kuanzia ngazi ya mtaa hadi taifa, pamoja na mchakato wa katiba.
Amesema kuwa maagizo ya mwenyezi Mungu,
yanatuelekeza kuacha kuwadanganya wasiojiweza, na yatima ili tuongoke, na
kuacha kutapeli mali za wanyonge kwa
kufisadi mabilioni ya fedha huku wakila chakula cha kawaida kama wengine, hali
ambayo amesema kuwa ni uonevu kwa wasiojiweza.
Ibaada ya ijumaa kuu husaliwa kote duniani, ambapo
wakristo hukumbuka mateso ya Yesu Kristo, hivyo waumini hutumia nafasi hiyo
kupinga matendo ya Yuda ambaye hakushiba mpaka alipojitundika.
Na Mwanaharakati.


No comments:
Post a Comment