MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday, 21 April 2014

DEREVA AMEVUNJIKA MIGUU NA WANANCHI KUTISHIWA KUPIGWA RISASI, BAADA YA AJALI YA GARI KUGONGANA


Daladala iliyogongana na Gari aina ya Nissani Hard Body muda mufi uliopita katika eneo la Suye barabara inayoelekea Moshono Mjini Arusha.

Nissan Hard Body ambayo namba yake ya usajili haikuweza kufahamika mara moja ikiwa imeharibika vibaya mara baada ya kusababisha ajali ya kugongana uso kwa uso na daladala katika eneo la Suye, Barabara ya kuelekea Moshono mjini Arusha leo asubuhi.
Ajali hiyo imetokea mjini Arusha katika eneo la Suye barabara ya Moshono, ambapo magari yaliyohusika ni Haice na Nissan Hard Body ambapo dereva la daladala amevunjika miguu.

Kutokana na ajali hiyo Dereva wa Nissan alitaka kukimbia wananchi wakamzonga akatoa Bastola kuwafyatua kwa risasi ndipo yakatokea machafuko yaliyosababisha barabara hiyo kufungwa kwa muda.

Taarifa zinasema kuwa dereva wa Nissan alikuwa amelewa na kusababisha gari yake kuyumba na kugongana na Daladala, na polisi walijitahidi kutuliza gahsia hiyo muda mfupi baada ya kuwasili kwao katika eneo hilo na anashikiliwa na jeshi hilo.


Na Mwanaharakati.

No comments: