
"Ukiangalia wajumbe wengi
wameweka maslai ya vyama na Taasisi zao na si Nchi kwani inaeleweka wazi
mada ya kudai Katiba mpya ilibebwa na baadhi ya Vyama vya Siasa na Taasisi
Fulani kwa lengo kudai muundo mzima wa kuunda Tume huru ya Uchaguzi"
"Lakini cha kuchangaza watu
hawa wameona na kukubali kutumiwa na Mataifa na Nchi za Mataifa ya Magharibi
kwa lengo la kuigawa Nchi yetu vipande vipande na kwa lengo la kundi
kutawala tena hususani kwa upande wa visiwa vyetu wakiamini havina ulinzi na
usalama mathubuti"
Kingine walichokizungumza ni kuhusu
Profesa Lipumba ambapo walisema:
"Kwa mfano Mh Prof Lipumba alipopokea taarifa za kuungwa mkono na baadhi ya Nchi ya Magharibi aliweza kufuata msimamo wake na kupinga makala aliyoitoa ya kuunga mkono muundo ulio asisiwa na hayati Mzee J.K. Nyerere na Mzee Karume."
"Kwa mfano Mh Prof Lipumba alipopokea taarifa za kuungwa mkono na baadhi ya Nchi ya Magharibi aliweza kufuata msimamo wake na kupinga makala aliyoitoa ya kuunga mkono muundo ulio asisiwa na hayati Mzee J.K. Nyerere na Mzee Karume."
Hii ni ratiba ya Maandamano na
Mikutano ya Hadhara itakayofanywa kikanda na Kamati ya Tanzania kwanza nje ya
Bunge.
1.
KANDA YA KASKAZINI (ARUSHA MH. DR
HALSON MWAKYEMBE NA SIXTUS MAPUNDA)
2.
NYANDA ZA JUU KUSINI (MBEYA MH. PROF
MWANDOSYA NA NDUGU ASENGA)
3.
KANDA YA MAGHARIBI (KIGOMA MH.
MWIGULU NA IDDI MAJUTO)
4.
KANDA YA KATI (DODOMA NA TABORA MH.
SAID NKUMBA)
5.
KANDA YA KUSINI (MTWARA MH. PANDU
AMIR KIFICHO)
6.
KANDA YA MASHARIKI (DSM MH. NAPE NA
MH. ABBAS MTEMVU)
7.
KANDA MWANZA (MH. PAUL MAKONDA NA
NDG MATEFU)
8.
ZANZIBAR (PEMBA MH. HAMAD RASHID NA
MH. RENATUS MHABI- KATIBU MKUU CCK (CHAMA CHA KIJAMII).
9.
UNGUJA (MH. MASAUNI NA MH. JUMA K.
SADIFA (KIBANDAMAITI
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment