![]() | |||
| Wananchi wakipiga kura katika kituo kimoja cha shule |
![]() |
| Ni katika ofisi za kata |
Upigaji kura huo umeendelea ilhali zikiripotiwa taarifa chache za vurugu.
Habari zimeeleza kuwa vijana hao wameletwa kwa ajili ya
kufanya vurugu, kupiga, kutesa, kuteka, kujeruhi na kuua wapinzani wa CC,
ambapo walengwa ni CHADEMA, kama ilivyo ada ya chama hicho tawala kufanya hivyo
kwenye chaguzi mbalimbali, hususan kinapokuwa kimezidiwa na kupata hofu ya
kushindwa, wamepiga na kujeruhi takriban watu 9.
Wakiwa kwenye operesheni ya kile
'walicholetewa' Chalinze, jioni hii, wamewakuta watu waliodhani kuwa ni
makamanda wa CHADEMA katika eneo la Msoga, wakaanza kuwashushia kipigo kikali,
kisha wapigaji hao wakakimbia.
Katika watu hao 9 waliopigwa na vijana hao wanaosadikiwa kuwa wa CCM, wamo maofisa wa UWT, mtoto wa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo na waandishi wa habari na watu wengine ambao hawajafahamika vizuri 'majukumu' yao kwenye msafara huo ambao leo ulikusanya watu wengi kwa kuwasomba kwa malori kutoka maeneo mbalimbali kwenda kujaza mkutano wa kufunga kampeni huko Miono.

Hatahivyo vijana hao walikamatwa wakiwa kwenye gari yao aina ya Land Cruiser 'hard top' ambapo ilipofikishwa kituo cha polisi 'mjini' hapa, limekutwa na mapanga, rungu, kamba, tindikali na petroli.
Kitu cha kushangaza katika tukio hilo ni kwamba vijana hao wameachiwa pamoja na gari lao na silaha walizokuwa nazo, bila kufunguliwa jalada la kesi, baada ya msemaji wa CCM kufika kituoni hapo na maelekezo maalum.
Waliopigwa na kujeruhiwa, inasemekana wamekimbizwa hospitalini Dar es Salaam, kwa maelekezo maalum
Na Mwanaharakati.

No comments:
Post a Comment