MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 6 April 2014

WATENDAJI 15 WASHIKILIWA NA POLISI GEITA

Jeshi hilo mkoani Geita linawashikilia watendaji hao wa kata 15 za wilaya ya Geita zinazotokana na halmashauri mbili za wilaya hiyo kwa kosa la kushindwa kuwakamata wazazi na walezi  kwa kushindwa kuwapeleka shule wanafunzi na darasa la kwanza wakiwemo na watoro sugu.
Askari polisi wakikamata wakiwa katika msako wa watendaji
Mkuu wa mkoa Geita Magalula Said Magalula
Agizo la kukamatwa kwa watendaji hao limetolewa juzi na mkuu wa mkoa wa Geita Bw Said Magalula kwenye kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita lengo likiwa kubaini ni watoto wangapi waliofaulu na hawajaenda shule na watoro sugu.

Bw Saidi aliongeza kuwa kuna wazazi ambao watoto wamefaulu kwenda sekondari lakini wazazi wanawaficha majumbani kwa ajili ya kuwafanyisha kazi mbalimbali na ikiwemo kuwaozesha kwa nguvu au kuwapeleka migodini kuchenjua dhahabu na wengine kuwapeleka kuchunga wakati kikao cha mkoa kiliagiza watendaji wa kata zote wanatakiwa kuwakamata wazazi waliofanya hivyo na kuwafikisha mahakani lakini mpaka sasa ni wazazi wachache waliotekeleza hilo.

Bw Saidi akaagiza kuwa kati ya kata 35 kwenye wilaya Geita ni kata 20 tu zilizotekeleza agizo hilo la kuwakamata wazazi na kuwafikisha mahakamani hivyo kuamuru watendaji 15 waliokataaa kutekeleza agizo hilo kuhakikisha wanakamatwa mara moja na kufikishwa mahakamani.

Lakini pamoja kukamatwa kwa wetendaji hao mwandishi wa habari hii aliongea na mmoja wa watendaji  ili kutaka kujua kwanini walikiuka agizo la mkuu wa mkoa , Bw Wiliam Rufungu ambambeye ni Mtendaji  wa kata chigunga alisema kuwa kwenye kata yake amekuwa na changangamoto kubwa kutokana na wazazi kuwaamisha watoto na kuwatorosha kwenda nje ya kata yake.
 Na Mwanaharakati.

No comments: