Wahanga wa mafuriko Wilayani Kilombero mkoani Morogoro wameiomba serikali kuwapatia misaada mbalimbali ikiwemo ya chakula pamoja na makazi .
Wakizungumza na mtandao huu, wahanga wa
mafuriko Wilayani humo wamesema wanaomba misaada ya chakula ili waweze
kupambana na hali hiyo.
Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari ya Tekfoti Mwl.Mohamed Majaliwa amesema kuna zaidi idadi ya kaya takribani ishirini ambao nyumba zao zimeondolewa na mafuriko .
Nae Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya
ya Kilombero Bw Daudi Ligazio amesema kwasasa wana mpango wa kuweza kuwasaidia
wahanga hususani katika msaada wa chakula .
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment