MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday, 21 April 2014

KIFO CHA DC KALAMBO HIKI HAPA

Marehemu Chang'a enzi za uhai wake
Taarifa iliyotolewa na mkuu wa mkoa wa Rukwa Muhandisi Stela Manyanya, zinasema kuwa marehemu mkuu huyo wa wilaya, aligua kisukari kwa kipindi kadhaa.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Bi Stella Manyanya.
Amesema kuwa alikuwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam, na kuwa msiba upo nyumbani kwake Mbagala Zakiem jijini humo, na taratibu za mazishi zinaendelea ambapo mwili utaagwa rasmi jumatano, 23 April 2014.

Kwa upande wake mtoto wa marehemu Bi Zainab Chang'a, amezungumza kwa niaba ya familia, kuwa wamepokea kifo cha baba yao kwa mstuko mkubwa, lakini hawana jinsi katika hilo, na kuwa wanaomba ndugu jamaa na marafiki kuiombea familia yao katika kipindi hiki kigumu, huku akisema kuwa baba yao hakuwa na kinyongo na watu.
Na Mwanaharakati.

No comments: