MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday, 17 April 2014

WAHAMIAJI 32 WAMEKAMATWA MKOANI KAGERA


Ni raia wa Burundi wamekamatwa mkoani kagera wakati wakijiandaa kusafiri kuelekea nchini Burundi na kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma.
Kamishna msaidizi George Kombe akizungumza na waandishi wa habari.

Ni baadhi ya wahamiaji haramu wakizungumza na Kamishna msaidizi wa Magereza.

Akizungumza na waandishi wa habari kamishna msaidizi mkoani Kagera George  Kombe, amesema kukamatwa kwa wahamiaji hao haramu kumefuatia taarifa zilizotolewa kwa idara hiyo kutoka kwa raia wema.

Amesema wahamiaji hao walikamatwa April 16, 2014 wakiwa wamepakiwa kwenye gari aina ya Toyota  AICE lenye nambari za usajiri T 633 CPZ lilowasafirisha kutoka eneo la Mtukura  mpakani wa Tanzania na Uganda.
Gari iliyokuwa imewabeba wahamiaji hao
KOMBE amesema taratibu za kuwasafirisha watuhumiwa hao zilikuwa zimekamilika na kueleza kuwa, ilikuwa wasafirishwe kuelekea maeneo ya mpaka wa Burundi mkoani kigoma.

Awali baadhi ya wakimbizi hao wamedai kuondoka pasipo kuaga katika kambi ya wakimbizi ya nchini Uganda wakidai kuwa maisha katika kambi hiyo yamekuwa magumu.

Wanasema kuwa wakimbizi katika kambi hiyo wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa kuni,maji, na chakula, huku wakilalamika kuwa misaada inayotolewa na mashirika mbalimbali ili kusaidia kambi za wakimbizi kwa kiasi kikubwa haziwafikii walengwa.

Wahamiaji hao wametokea kambi ya Nyakivala nchini Uganda wakielekea Nyalugusu, baada ya kupata taarifa kuwa wakimbizi wa pale wamepata fursa ya kwenda kuishi Uingereza, wengine walitaka kwenda Burundi baada ya kukosa huduma sahihi katika  kambi ya Nyakivala.
  Na Mwanaharakati.

No comments: