
Kingine kikubwa alichozungumza Prof.
Lipumba ni kusikitishwa na kauli ya Waziri Lukuvi aliyoitoa kanisani weekend
iliyopita kwamba jeshi litatawala nchi ambapo April 14 2014 gazeti la Mwananchi
lilimnukuu Waziri Lukuvi akisema Kanisani ‘tukipitisha serikali tatu jeshi
litatawala nchi’
‘Ni kweli kwamba kikao hichi
nilipanga nisichangie kwa sababu niliona mechi kali tukishindilia watu
watakufa, sikusikia vizuri yaliyotokea jana ila mimi sio mnafiki, nampongeza
sana Mh. Mrema kwa hotuba yake juzi, Mrema ndio mpinzani wa kweli, alisema
angalia mambo yanayotokea Znz msidhani yataishia Magogoni’
‘Baada ya hotuba ya Rais, mh. Seif
Sharrif Hamad alihutubia, yeye ni mchochezi wa hovyo kwa kumsingizia Rais,
hakuna mtu yeyote anaweza kunizuia kusema ninayoyaamini mimi, sio hapa wala
mtaani, ni kweli Jumamosi nilimwakilisha Waziri mkuu ambae hakunipa hotuba na mambo
yalinoga nikatawazwa kuwa chifu’
‘Viongozi wa dini waliliombea Bunge
pale Kanisani, mimi Waziri nipo pale… nisiongee chochote??!! tukiendeleza
ambayo hayako kwenye mila zetu Znz na Tanganyika inaweza kuwa kama Korea
kaskazini na kusini, hofu niliyonayo ni juu ya rasimu yenyewe kwa sababu kwanza
imejengwa kwenye misingi ambayo siiamini’
‘Zanzibar inatambulika kama nchi
kwenye katiba yao toka hata kwenye katiba ya nyuma kabisa, yapo mapungufu
muundo wa serikali 3, ukisoma rasimu wanasema serikali ya Tanganyika imevaa
koti la muungano lakini koti lenyewe tunapokezana, leo anavaa Mwinyi, leo
anavaa huyu’
‘Hatujawahi kutoa bajeti inayotosha
kwa jeshi la Wananchi, mmeshawahi ona wanaandamana kudai haki zao? nina miaka
zaidi ya 50 na nisingependa kuiona Tanzania hii inakwenda kwenye maisha ambayo
sikuyazoea ili kuepusha haya tusijaribu tusichokijua, hii ni hofu yangu… hakuna
wa kunizuia kutoa hofu yangu’
‘Ukweli ni kwamba kama umesoma hii
rasimu, muundo unaweza kuwa umeandikwa vizuri lakini hauwezi kuwepo, Rais
hakutoa vitisho bali mawazo yake kama Mtanzania, hawa jamaa wamekubaliana,
serikali ya Znz wachukue CUF, bara CHADEMA na muungano waachiwe CCM’
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment